Serikali imetakiwa kuboresha Mahabusu ya watoto iliyopo Upanga, Dar es salaam kutokana na udogo wa mahabusu hiyo. Hayo yamesemwa mapema leo bungeni, ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 serikali imetenga zaidi ya bilioni 2 kwaajili ya kuboresha makazi ya wazee na kuboresha nyumba za kuboresha nyumba za kurekebisha tabia watoto.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema Serikali itaimarisha maeneo ya Magereza na Mahabusu, pia amesema Serikali inajenga mabweni mapya na kupanua na kufuatia bajeti ya takribani bilioni 3 iliyopitishwa kwaajili ya kazi hiyo itahusisha ukarabati wa mabweni 15 katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kuimarisha hudumakatika Magereza. Tazama hapa Video

Mambo ya kuzingatia katika kupiga hatua kimaisha
Obama akutana na Rais wa Ufilipino aliyemtukana tusi ‘zito’