Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itafufua viwanda vyote vya chai vilivyokuwa havifanyi kazi ili wakulima wanaolima chai wapate sehemu za kupeleka mazao yao, wapate fedha na kuendelea na kilimo.
Majaliwa amesema hayo wakati alipotembelea wakati alipotembelea kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.
“Lupembe ni miongoni mwa viwanda ambavyo vilikufa na sasa kimeanza uzalishaji hatutakubali kife kutokana na migogoro ya wanaushirika na muwekezaji. Kiwanda hakitasimama ng’o,” – Majaliwa.
Aidha, Majaliwa amewataka wawekezaji mbalimbali waliomilikishwa viwanda wahakikishe wanafuata kanuni na sheria ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na wananchi waweze kupata tija.