Serikali imepanga kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Ngungungu – Mamire wilayani Babati, mkoani Manyara ili uweze kurahisisha mawasiliano kwa mikoa mitano inayozunguka mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na watumishi na viongozi mbalimbali wa mkoa huo kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani Manyara ambapo ameeleza kuwa upembuzi yakinifu ili kubaini gharama za ujenzi wa uwanja huo utafanyika mwaka 2019 na ujenzi halisi utaanza katika bajeti ya mwaka 2020/2021.

“Tumechagua eneo la Ngungungu-Mamire kwa sababu liko karibu na mbuga za wanyama; lakini pia tuna hospitali yetu kule Haydom ili kama kuna mgonjwa amezidiwa iwe rahisi kumpakia na kumpeleka kwenye hospitali za rufaa.”

Afrika Yapendekeza Kuongezewa Timu Kombe la Dunia
Man Utd Yatangulia 16 Bora Europa League