Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali inaendelea kukamilisha mifumo na ujenzi wa miradi mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wa umma ambao watahamia na kufanya kazi katika majengo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaofika katika mji huo wa Serikali, ikiwa ni sambamba na kuboresha jiji la Dodoma.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara itakayogharimu bilioni 500 kwa mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayojengwa kutokea Mtumba, Veyula na Nala ambayo ina urefu wa kilomita 4.

Vile vile amesema, Serikali inaendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa na wa kimataifa unaogharimu bilioni 400 pia inafanya maandalizi ya ujenzi wa  Bandari kavu kwa vile jiji la Dodoma lina kituo kikuu cha reli ya kisasa (SGR).

Katika jitihada za Serikali za kuliboresha jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya nchi, Serikali imepanga kujenga shule ya sekondari ya kisasa itakayogharimu shilingi bilioni 13 na Chuo cha mafuzo (VETA) kitakachogharimu shilingi bilioni 18. Ikiwa ni pamoja na kuendelea kuimarisha hospitali ya Benjamini Mkapa ambayo imeanza kutoa matibabu ya kibingwa.

Video: Hakuna kinachonichelewesha kuhamia Dodoma, nakuja - Rais Magufuli
Treni ya mizigo yapata ajali