Serikali imetangaza kutoa onyo, kuvifungia vyuo vyote vya Tanzania vinavyotoza ada za kigeni kwa wanafunzi. Hayo yamesemwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Eng. Stella Manyanya wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Tumbatu, Juma Othman Hija.

Naibu waziri amesema tayari Serikali imeshavionya baadhi ya vyuo vya IMTU na KIA kuhusu kutoza fedha za kigeni, huku akisema vyuo huvyo vinaweza kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa wanafunzi wasiyo Watanzania na siyo watanzania kwa mujibu wa Sheria. Hii hapa video kutoka Bungeni

Kampuni ya Apple yatoa tolewa jipya iphone 7
Serikali inafikiria nini kuhusu deni la taifa?