Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haitamsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhilifu wa mali za fedha za Ushirika nchini.

“Kwa Serikali hii ya awamu ya Tano tutachua hatua kali kwa wezi wa mali na fedha za ushirika na tunaendelea kufanya usafi wa wabadhilifu hadi tupate viongozi waadilifu,”.

Majaliwa amesema hayo leo Julai Mosi, 2017, katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD), iliyoadhimishwa kitaifa mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Amesema miongoni mwa changamoto zinazoukabili Ushirika nchini ni pamoja na wizi na ubadhilifu wa rasilimali za Ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wasiokuwa waaminifu.

“Haikubaliki hata kidogo kuona sekta hii inayosadifu maisha ya Mwafrika hamnufaishi ipasavyo , hivyo naelekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ihakikishe kuwa vyama vya Ushirika vinaendeshwa kisayansi na kwa mujibu wa sheria,” amesema.

 

Mrisho Mpoto ateuliwa kuwa balozi wa utalii
Kamati ya utendaji ya TFF yakutana, yatoa maamuzi magumu kuhusu Malinzi