Serikali imekusanya Madini yenye thamani ya dola za Marekani milioni 10.86 na mengine yenye thamani ya shilingi bilioni 1.28 katika matukio 100 ya utoroshaji wa madini hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Habari toka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa Serikali kupitia madawati ya ukaguzi yaliyopo katika viwanja vya ndege nchinj, kwa kushirikiana na taasisi zingine za serikali, umekuwa ukiwakamata watu wasio waaminifu wanaojaribu kusafirisha madini nje ya nchi kinyume cha sheria.
Hata hivyo, Yisambi amesema kuwa Wakala umejipanga na ukaguzi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini ili kuhakikisha Serikali inapata mapato stahiki.