Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya upatikanaji wa Dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja mbalimbali za Wabunge leo Mjini Dodoma.

Amesema kuwa katika kutekeleza azma hii Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia bilioni 251,500,000,000 katika mwaka wa fedha 2016/17.

“Moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma nchini,”Amesema Dkt. Kigwangalla.

Hata hivyo, ameongeza kuwa hadi kufikia Mwezi April 2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.

 

Video: Majaliwa atembelea kiwanda cha sukari cha TPC
Stand Utd Waapa Kuzikaba Koo Simba SC, Ruvu Shooting