Serikali imeunga mkono mikopo kwa Wasusi ambayo inatolewa bila  mkopaji kuwa na dhamana ya Mali.

Akizungumza katika semina maalumu ya Wasusi iliyoandaliwa na kampuni ya Kopafasta ambavyo inatoa mikopo kwa makundi yaliyokuwa hayakopesheki Kama wasusi, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, Afisa Tawala wa Wilaya ya Kinondoni kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Editha Elias amesema kuwa serikali inaunga mkono dhumuni lao la kukopesha wasusi.

”Sisi kama Serikali tunaahidi kufanya kazi bega kwa bega na Kopafasta ili  kuhahakikisha hii inamfikia kila mtu anayehitaji kwani wanaohitaji ni wengi lakini hawajui cha kufanya” amesema Editha

Kwa upande wake Meneja wa kopafasta, Patrick Kang’ombe amesema wamelenga katika mtazamo chanya wa kuyakwamua makundi ambayo yapo katika sekta isiyo rasmi Kama sanaaa na moja ya makundi hayo ni Wasusi ambao wamekuwa hawakopesheki na wanakabiliwa na changamoto nyingi…, Bofya hapa kutazama

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 22, 2019
Benki ya dunia kuipa Tanzania dola bil. 1.7