Serikali kwa kushirikiana na Mashirika  ya USAID,MFDI, wamezindua Program ya kumekucha chini ya mradi wa wanawake na vijana katika kilimo Tanzania ambao utakua unarushwa na vituo mbalimbali vya redio hapa nchini.

Uzinduzi huo umefanyika mapema hii leo jijini Dar es salaam na kuhudhuliwa na Mkurugenzi wa mawasiliano kutoka Wizara ya Kilimo Bw, Richard Y Kasuga ambae alimuwakilisha katibu mkuu wa Wizara ya kilimo,uvuvi na umwagiliaji.  .

Kwa upande wake mwakilishi wa USAID bw, Randy Chester amesema kuwa  sheria na tamaduni zilizopo zinakwamisha juhudi za wanawake kupata fursa za kiuchumi kwakua hawana haki ya kumiliki ardhi na ukosefu wa mikopo wanayohitaji ili kufanikisha juhudi zao hivyo kukwamisha maendeleo kwa wanawake.

Aidha Program hiyo ya kumekucha imewashirikilisha wasanii mbalimbali wakiwemo wakongwe na waliowahi kucheza filamu kama vile siri ya mtungi,wa hapahapa na chipukizi katika tasnia hiyo ya uigizaji na kutoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao.

Hata hivyo kwa upande wa Serikali kupitia mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo  bw, Richard Kasuga alisema kuwa  serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanya jitihada kubwa  kama vile; kutunga sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007, yenye lengo la kuwawezesha na  kuwaelekeza vijana na wadau katika kujihusisha na shughuli za maendeleo ya vijana ikiwemo kilimo.

Kutunga sera ya taifa ya ajira  ya mwaka 2008 na program ya taifa ya  kukuza ajira (2006-2010) kutambua kilimo kuwa moja ya sekta  zinazo ongoza kutoa ajira kwa wingi, sera ya maendeleo ya kilimo ya 2013 pamoja na mambo mengine inahimiza kuweka mazingira wezeshi kuwavutia vijana na wanawake katika kilimo.

Program hiyo itakua inarushwa na vituo vya redio free Africa, Ebony fm, Bomba fm, Abood fm kwa lengo moja tu la kuelimisha jamii kuhusu haki ya mwanamke katika kilimo na kuishawishi jamii kumthamini mwanamke

Video: Mawaziri Watakiwa Kuhamia Dodoma Mara Moja
Mapacha wa P Square watangaza rasmi kumaliza ‘bifu’ kati yao