Shirika la Posta Nchini limetoa msaada wa shilingi millioni 4 kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kuchangia matibabu ya Moyo kwa watoto wawili wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo.
Hayo yamesemwa na Posta Master na Mkjurugenzi Mtendaji wa Shirika la Posta jijini Dar es salaam, Deo Kwiyukwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Shirika limeaamua kuadhimisha siku ya Posta duniani ambayo inafanyika octoba 9 kila mwaka, kwa kusaidia matibabu ya watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo.
“ Tunafahamu matibabu ya magonjwa ya Moyo ni gharama hivyo sisi kama Shirika la Posta tukaona ni vyema tuchangie japo kidogo kwenye matibabu ya Moyo kwa watoto kama maadhimisho ya siku yetu badala ya kuiadhimisha ofisini kama ilivyokuwa zamani”,Alisema Kwiyukwa.
Amesema kuwa Shirika hilo linaunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta Afya Bora kwa Wananchi wake na inafurahi kuona katika siku yao wataweza kurudisha tabasamu kwa watoto japo wawili wenye matatizo ya Moyo.
-
Miili yaopolewa Ziwa Victoria
-
Waziri Mkuchika aanza kwa kutoa onyo kwa watumishi
-
Mbowe asikitishwa na kauli ya Kardinali Pengo
Hata hivyo, Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyoya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohammed Janabi amelishukuru Shirika hilo kwa msaada huo kwasababu utawawezesha watoto wawili kutibiwa kwani gharama za matibabu ni kubwa.