Ni mara chache sana kwa vijana kuamua kuandika wimbo unaolenga kuelimisha jamii, mara nyingi sana tumekuwa tukisikia nyimbo za mapenzi au ‘ku-bang’ na kujirusha lakini kwa namna ya kipekee kabisa kikundi cha Muziki cha Kiswahili na Sanaa (KINASA) wamekuja na wimbo unaoelimisha juu ya matumizi ya madawa ya Kulevya.
Wimbo huo unaofahamika kama Narudi nyumbani ambao ndani yake umekuwa ukielezea kuwa mwathirika wa madawa sio muhalifu, anahitaji kusaidiwa na sio kutengwa, anahitaji kuheshimika na kuthaminika. Wimbo huo ulioandaliwa na Tanzania Bora Initiative chini za mzalishaji mahiri anyefanya vizuri kwenye game ya muziki (Mocco Geneius) na video kufanya na Adam Juma ambaye ni miongoni mwa ma-director wakubwa sana nchini Tanzania.
Tazama hapa kuona kile ambacho vijana wa kitanzania wanaweza kufanya kwa ajili na vijana wenzao na nchi yao.