Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepokea vitanda 150 na magodoro 150 vyenye thamani ya shilingi milion 300 kutoka Kampuni ya Mafuta ya Camel ili kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha sekta ya Afya.
Amesema kuwa vitanda hivyo vitapelekwa kwenye Wodi mpya ya Mama na Mtoto iliyojengwa kwenye Hospital ya Amana ili kuweza kupunguza msongamano wa akina mama kulala katika kitanda kimoja.
“Sitaacha kutafuta kwaajili ya Wananchi wangu wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ili mradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri,” amesema Makonda.
Aidha, ameongeza kuwa amedhamiria kuhakikisha kuwa Mama, mtoto na wananchi wote wa Mkoa wa Dar es salaam wanapata huduma bora katika hospital zote za mkoa wa Dar es salaam.
Kwa upande wake Meneja uendeshaji wa biashara Kampuni ya Camel Oil, Suleiman Amour amesema kuwa vitanda hivyo ni muendelezo wa kutoa mchango wao wa kuunga mkono juhudi za mkuu huyo wa mkoa