Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, siku ya mwisho wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Barani Afrika (AU), alikutana na marais mbalimbali wa Afrika na kufanya nao mazungumzo katika suala la maendeleo.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli na alikutana na marais hao kwa nyakati tofauti tofauti na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uwekezaji na mahusiano ya kibiashara na kukubaliana kuunda kamati ya pamoja ya viongozi wa juu ili waweze kusaini mikataba mbali mbali itakayowezesha kukuza biashara.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemkaribisha rais wa Misri kuja kuwekeza katika viwanda vya dawa hapa nchini na kushirikiana katika masuala ya kilimo na kupeana uzoefu.

Pia amekutana na rais wa benki ya maendeleo ya Afrika na kukubali kusaidia mipango ya nishati,barabara,viwanda na mambo mabalimbali na kuwataka benki hiyo kuja na mipango mizuri ya kuisaidia Tanzania.

 

AFCON 2017: Ghana Italipa Kisasi Cha Mwaka 2008?
AFCON 2017: Mwamuzi Bora 2016 Kuamua Ghana Vs Cameroon