Msanii wa muziki na filamu ‘Bongo’, Sister Fay amesema kuwa kama angekuwa hajaolewa msanii wa Bongo Fleva ambaye angetamani amuoe ni Naseeb Abdul maarufu kama, Diamond Platinumz kwani ni moja ya wanaume wapambanaji ‘bongo’.

Aidha, amezungumza kuhusu ukimwa wake katika mitandao ya kijamii mara baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba wake Holy Star ambaye waliachana mara baada ya kutangaza kuwa wawili hao hawakuwa kwenye mahusiano bali ilikuwa ni kiki.

Sister Fey amesema kuwa sasahivi ameachana na mambo ya kiki kwani mume wake tayari  amerudi.

”Sasahivi mambo ya makiki nimeachana nayo mume wangu amerudi kutoka aliko toka sasa yupo Tanzania”. amesema Sister Fay.

Tazama video nzima hapa.

Video: Anasumbuliwa na maradhi makubwa matatu, mwenyewe asimulia "Muda wowote nakufa, Mungu anaweza''
Steve Nyerere: 'Nilisikia pua zinatanuka Mlima kilimanjaro sio Mlimani City'