Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa kamwe hawezi kuomba radhi kwa tukio lilitokea Clouds Media Group (CMG) kwa sababu hukumu iliyotolewa na Jukwaa la Wahariri ilikuwa ya upande mmoja.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo amesema hukumu hiyo ilikuwa ya upande mmoja hivyo hilo lilikuwa ni jambo lake yeye kumalizana na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.
“Nimesema sitaomba msamaha kamwe, kwa suala hili, kwani kile kilichosemwa kuwa nimevamia Clouds Media sio cha kweli, tafsiri ya neno uvamizi ni kubwa sana, wala TEF hawana makosa kutoa hukumu yao kwakuwa walisikiliza upande mmoja,”amesema Makonda
-
Serikali yatoa onyo dhidi ya wananchi wanaouza ardhi
-
Video: Ruge azungumza haya baada ya kukutana na Makonda, Jukwaa la Wahariri
Hata hivyo, ameongeza kuwa hakuna haja ya kuendelea na malumbano yasiyokuwa na msingi wowote, kwani adhabu iliyotoka tayari ilishachukuwa ya muda mrefu hivyo ni bora ikaisha.