Msanii wa bongo fleva Barnaba anayemiliki lebo ya muziki amekiri kusaidiwa na baadhi ya wadau akiwepo marehemu Ruge Mutahaba katika kuendesha maisha yake ya muziki hivyo ameamua kusaidia vijana wengine katika kufikia ndoto zao kimuziki kama ambavyo King Music, wasafi walivyowasaidia baadhi ya vijana kwa kufungua lebo ya muziki.

Na kutokana na hali ya baadhi ya lebo zilizowahi kufunguliwa na baadaye zikakwama, kwa upande wake amesema hategemei lebo yake kukwama.

”Sitegemei kukwama katika lebo yangu kama ambavyo wengine wamekwama , hata hivyo sijakutana na changamoto tusubirie bidhaa  iingie sokoni kwani zile ni ‘product’ hazitembei kama watu wanvyotaka” amesema Barnaba.

Video: "Sijamsaini Q Chief, nimemsaidia gari" - Harmonize
Video: Fahamu lishe bora kwa mtoto baada ya miezi 6

Comments

comments