Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema kuwa tuhuma zinazomkabiri za kuwapiga mawe Polisi si za kweli bali wameamua kumbakia kesi.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa yeye hawezi kufanya kitu kama hicho.
Amesema kuwa yeye kama mwanasiasa hajawahi kufanya tukio lolote la uvunjifu wa amani, hivyo jeshi la Polisi linatakiwa kujitafakari kabla ya kutoa tuhuma hizo.
“Katika maisha ya kawaida sana, sifanani hata kidogo kuinama na kuokota mawe kuwapiga polisi, hizi tuhuma wananibambikiza, wanampango wakutufunga kifungo cha muda mrefu,”amesema Mnyika