Mwanasheria kijana na Wakili wa Kujitegemea, Leonard Manyama amesema kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alitumia mamlaka yake vizuri kumfutia ubunge, aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa sheria iliyotumika kumfutia mbunge huyo iko wazi kwasababu alikuwa amekiuka utaratibu wa bunge.

”Kama mbunge akishindwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge, sheria iko wazi, nasikia kuna watu wanalalamika kuwa Spika Ndugai hajatenda haki kuhusu maamuzi, hii sio kweli yale sio maamuzi yake bali ni sheria ndio inasema hivyo, Spika yeye ni mtekelezaji tu,”amesema Wakili Manyama.

NGO's zaonywa, 'Ole wake atakayeenda kinyume na matakwa ya Serikali'
Serikali mkoani Kagera yatenga zaidi ya mil. 20 kwaajili ya Vijana