Jana Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji walilipoti kituo cha Polisi cha Kati ikiwa ni kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda la kuwataka walipoti kituoni hapo kufuatia majina yao kuwepo kwenye orodha ya watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amezungumza na waandishi wa habari leo Februari 10, 2017 na kueleza kinachoendelea kuhusu watuhumiwa hao pamoja na wengine ambao wametakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano. Bofya hapa kutazama video