Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Juma Kaseja, Erasto Nyoni na Adi Yusuph kwa niaba ya wenzao wamewaomba wadau wa soka nchini kuendelea kuwaunga mkono katika harakati za kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022.

Taifa Stars ilifanikiwa kuiondosha Burundi kwenye mbio za kuwania nafasi ya kushirki kombe la Dunia kwa mikwaju ya penati 3-0 baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ambapo mchezo ulipigwa septemba nane kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 11, 2019
Baada ya kuifyeka Burundi, TFF yajipanga dhidi ya Sudan