Mwezi wa pili kila mwaka ni mwezi wa kuonesha upendo kwa watu wetu wa karibu na jamii kiujumla, na kawaida Februari 14, kila mwaka huwa ndiyo siku maalumu ya kusherekea siku ya wapendanao.

Kila nchi huwa na tamaduni zake za kusherekea siku hii ikiwa ni pamoja na kupeana zawadi mbalimbali kama vile maua, kadi, pipi, manukato, mvinyo na nyingine nyingi.

Kwa nchi ya Italia hapo zamani siku hii ilikuwa inasherekewa tofauti ambapo wanawake hutakiwa kuwa makini sana na wanaume kwani unaambiwa kwamba kwa siku ya valentine, mwanaume wa kwanza kutiwaa machoni pa mwanamke katika siku hiyo ni lazima mwanamke huyo aolewe na mwanaume huyo.

Na ndoa hiyo inatakiwa kufungwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Hivyo kama sheria hii ingekuwa inatumika hapa nchini kwetu, je wewe ungeoa au ungelewa na nani?.

Tazama video hapa chini.


Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 16, 2019
Video: 21 Savege azungumza aliwekewa mtego kukamatwa