Tanasha Dona Oketch ambaye ni mtangazaji wa NRG Radio nchini Kenya na mpenzi wa sasa wa msanii mkubwa nchini Diamond Platinumz mapema leo hii ameachia ngoma yake inayoenda kwa jina la Jacuzzi.

Huko nyuma amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kupost vionjo vya nyimbo hiyo ambayo leo ameiachia rasmi, nyimbo hiyo inauwezekano mkubwa wa kufanya vizuri kutokana na uhusiano wa karibu na Diamond Platinumz hali ambayo kwa kiasi kikubwa itamsaidia ngoma yake kufanya vizuri.

Tayari chaneli ya Wasafi TV imeupromote wimbo huo kwa kuupiga katika chaneli yao huku bosi wao Diamond Platinumz akiwa bado hajaupromote wimbo huo wala kusema chochote juu ya ujio wa wimbo huo.

Aidha mama Diamond Platinumz amempost na kuusifia ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika.

”Kama umetisha vile Mrs” ujumbe huo akiusindikiza na kipande kidogo cha video ya wimbo wa Tanasha.

Aidha Tanasha alipata nafasi ya kujibu ujumbe huo na kumshukuru mama Diamond na kumwambia anampenda.

”Thanks you so much mama .Love You” Tanasha amemjibu mama Diamond

Tanasha anatajwa kuwa ndiye mke mtarajiwa wa Diamond na hivi karibuni wanatarajia kufunga pingu za maisha.

Mchungaji aua waumini kwa kuwanywesha JIK
Kambi za Kitaaluma mkoani Simiyu ni za kudumu- RC Mtaka

Comments

comments