Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ametembelea jengo ambalo lilitumiwa na vyama vya kupigania ukombozi barani Afrika lililopo jijini Dar es salaam na kuwataka watanzania kutunza na kuheshimu sehemu mbalimbali za kihistoria.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea jengo hilo, ambapo amesema kuwa limejengwa hata kabla ya Tanganyika kupata uhuru, mwaka 1958 baada tu ya Ghana kupata uhuru.

Amesema kuwa viongozi mbalimbali kutoka Afrika akiwemo Nyerere waliunda waliunda chama chenye nguvu kwa ajili ya kupigania uhuru ndani ya bara la Afrika kilichojulikana kwa jina la PAN Africanism.

 

China yaimarisha uhusiano na Tanzania, yatoa mamilioni
Video: Lowassa amenifundisha mengi- Bashe