Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 yatwaa ubingwa CECAFA kwa kuifunga timu ya Kenya kwa bao 1-0, bao ambalo Kenya walijifunga kupitia mchezaji wao John Otieno Onyango.

Ambapo baada ya Tanzania kutwaa ubingwa huo, Kelvin John ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga mabao saba katika michezo mitano aliyocheza pamoja na kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 6, 2019
Tanzania yatwaa ubingwa CECAFA