Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan ambaye alifariki mwezi Agosti, 2018 jana majira ya jioni uliwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ghana unaojulikana kama Kotoka uliopo jijini Accra,

Mwili wa Kofi Annan uliwasili kutoka Uswisi na kupokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa nchi hiyo Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.

Mwili huo ulibebwa na Maofisa wa Umoja wa Mataifa ukisindikizwa na Mke wa marehemu Annan, Nane Maria Annan pamoja na familia yake.

Mara baada ya kuwasili mwili ulihifadhiwa katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano nchini Ghana kwa maombolezo ya siku tatu huku ukisubiri kuzikwa.

Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na Katibu mkuu wa 7 wa umoja wa mataifa ambaye ameleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika na dunia nzima kiujumla.

Kofi Annan alizaliwa Aprili 8, 1938 Kumasi katika mkoa wa Ashanti huko nchini Ghana.

Mkuu wa shirika la habari ajiuzulu kwa kashfa ya ngono
Tetesi za penzi la Tiwa Savage na Wizkid zamuamsha mumewe wa zamani