Kama bado hujatazama ngoma mpya ya Vanessa Mdee akiwa amemshirikisha Rayvanny inayoenda kwa jina la ‘Bado’.

Nimekuwekea hapa chini kuwa wakwanza kuitazama, ngoma hiyo ambayo imeachiwa rasmi  Oktoba 17, 2019.

Kama ilivyokawaida ya ubunifu mkubwa alionao Vanessa Mdee katika utayarishaji wa ngoma zake hasa upande wa picha mjongeo, amecheza kama yupo mbele, amejiachia, amevaa uhusika, ameimba kwa hisia kuendana na wimbo wenyewe.

‘Bado’ ni ngoma yenye maudhui ya mapenzi inayoelezea wapenzi ambao wamekuwa na hisia na upendo mkubwa.

Vanessa Mdee maarufu kama V Money ni moja ya wanamuziki mashughuli nchini Tanzania wanayoipeperusha vyema bendera ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwenye muziki wa ndani na nje ya Tanzania akifuatiwa na Nandy.

Tazama hapa chini, kisha weka komenti yako

Asilimia 25 ya mazao Duniani yanaathiriwa na sumukuvu
Menina ajisalimisha BASATA