Chama cha wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao na Mawasiliano (TEWUTA) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kwa agizo la kuitaka kampuni ya simu ya Airtel kuanza kuchunguzwa.

Hayo yamesema hii leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Junus Ndaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa chama hicho kimefurahishwa na uamuzi wa Rais wa kutaka kutatua suala hilo ambalo wamelilalamikia kwa mda mrefu.

Amesema kuwa uamuzi huo umewagusa Watanzania walio wengi hasa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwani imekuwa faraja kubwa kwao kwa kuleta matumaini mapya kwa kushuhudia kampuni yao iliyoanzishwa kwa mtaji na jasho lao ikirejeshwa na kuwa mali ya Umma baada ya kuporwa bila aibu na viongozi waliokuwa hawana uzalendo.

“TEWUTA kupitia kumbukumbu zetu za chama kwa miaka mingi tangu 2005 tuliwasilisha malalamiko yetu kufuatia kuporwa kwa kampuni ya simu Tanzania lakini malalamiko hayakupata majibu, tunamshukuru kwa dhati Rais Magufuli kuamua kufuatilia hili”, amesema Ndaro.

Aidha, chama hicho kinampongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya simu Tanzania, Mhandisi Omary Nundu kwa kuwa tayari kuthibitisha uhalali wa kampuni ya simu ya Airtel.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Makuke amesema kuwa TTCL haikupora kampuni ya Airtel pekee bali ilinyang’anywa pia Chuo cha Posta na Simu kitendo ambacho kilisababisha wafanyakazi wake kukosa mahali sahihi kwa kupata mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma.

Hata hivyo, TTCL ilibinafsishwa kwa mwekezaji wa nje mwaka 2001, wakati huo kampuni hiyo ilikuwa imeshaanzisha kampuni ya simu za mkononi kwa jina la CELNET, baada ya kuingia kwa wawekezaji kampuni hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa CELTEL ambayo iliwezeshwa na TTCL kimtaji, kiufundi, kimiundombinu na hesabu zake zilikuwa zikikaguliwa pamoja.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 29, 2017
Waliopiga mali za CCM matumbo joto