Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa tayari limeandaa mikakati ya kuhakikisha fainali za 2019 Taifa Stars inafanya vizuri na kufuzu.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas wakati akifanya mazungumzo na Dar24 ofisini kwake jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa kabla makundi hayajatangazwa TFF ilikuwa imeshajiandaa ikiwa ni pamoja na kuzungumza na kocha mkuu wa timu ya Taifa, Charles Boniface Mkwasa ili kuvunja mkataba na hatimaye ashike kijiti hicho kocha mwingine.

Amesema katika mazungumzo hayo Mkwasa amekubali na tayari ameteuliwa, Salum Mayanga atakaye iongoza timu ya Taifa akikaimu nafasi hiyo hadi atakapo patikana kocha mpya.

Aidha, Afisa habari huyo ameizungumzia michuano ya AFCON2017 ambayo imeshafunguliwa, amesema kuwa matumaina ya timu ya Taifa kushiriki michuano hiyo yalikuwa makubwa sana yaliyokwamishwa na kitendo cha timu ya Taifa ya Chad kujitoa katika michuano hiyo.

Samia: Wasaliti ndani ya CCM wachukuliwe hatua
Mkapa atoa neno kuhusu mapambano dhidi ya ujangili