Mtandao wa wanawake Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefungua warsha ya siku tatu kwaajili ya kujitathmini na kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali likiwemo suala zima la maji ili kuweza kumkomboa mwanamke.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi, alipokuwa akifungua warsha hiyo ya siku tatu, amesema kuwa lengp kubwa la warsha hiyo ni kujadili mambo mbalimbali ya kimataifa na kuangalia jinsi ya kutatua tatizo la maji kwa wanawake.
Amesema kuwa tatizo hilo ni kubwa kwa mwanamke hivyo ni lazima litafutiwe ufumbuzi ili kuweza kupunguza kero inayomwandama mwanamke.
Aidha, amesema kuwa pamoja na hilo pia watajadili masuala mbalimbali ya mikataba ya kimataifa iliyojitokeza kuhusu wanawake na kuangalia namana ya kuweza kushuriki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Maji Tanzania ( TAWASANET), Amina Malima amesema kuwa lengo namba sita linasema ni kuhakikisha upatikanaji na usafi wa mazingira kwa Mwanamke na kwawawezesha wakina mama kuishi maisha stahiki.
Amesema kuwa fedha zinazotolewa na serikali bado ni kidogo ambazo hazitosherezi katika usimamizi wa miradi ya maji na kuthamini huduma zilizopo.
Naye Mwanzilishi wa TGNP Aseli Muro, amesema kuwa hali halisi ya maji ni mbaya na bado hairizishi katika jitihada zake katika kusimamia miradi ya maji, amesema kuwa tanzania haijali haki za wananchi ya upatikanaji maji kama huduma muhimu katika jamii.