Msanii wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed maarufu kwa jina TID, leo ameungana rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es  salaam, Paul Makonda katika Kampeni ya kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya na watu wanaojihusisha na biashara hiyo ili iweze kutokomezwa.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda,  aidha TID ameomba msamaha kwa watu wote aliowakosea kipindi alichokuwa akitumia madawa hayo na kuahidi kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa za kutokomeza tatizo hilo la madawa ya kulevya.

Amesema kuwa vijana wengi wanateseka juu ya utumiaji wa madawa ya kulevya na kuangamia pasipo na sababu yeyote ya msingi, hivyo amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha Kampeni hiyo, pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kutilia mkazo Kampeni hiyo ya kupambana na madawa ya kulevya.

“Namshukuru Rais wetu Dkt. John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kuamua kutusaidia sisi vijana ambao tulikuwa tumejiingiza kwenye janga hili la utumiaji madawa ya kulevya, namimi kuanzia leo naungana rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam katika Kampeni hii, naamini tutashinda,”amesema TID.

Nape: Tumuunge mkono JPM vita dhidi madawa ya kulevya
Pep Guardiola: Sina Uhakika Kama Aguero Atabaki