Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amesema kuwa taasisi hiyo inawatambua wachimbaji wadogo wadogo wa madini kama wafanyabiashara.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Dar24Media mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini ulioandaliwa na wizara ya madini.
Amesema kuwa kwasasa wameanzisha kitengo maalumu cha kuwatambua wachimbaji hao, hivyo kuwatengenezea mfumo mzuri utakaowawezesha kutambulika kirahisi sehemu zao za kazi.
“Unaju hapo awali tulikuwa tunafanyakazi hasa na wachimbaji wa madini wale wakubwa tu, lakini kwasasa tumeunda mfumo maalumu wa kushirikiana na hawa wachimbaji wadogo wadogo wa madini, lakini sisi hatuwatambui kama ni wadogo, sisi tunawaita hawa wote ni wafanyabiashara,”amesema Simbeye