Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 15.5 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kuanzia julai 2017 hadi juni 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 14.4 ambazo zilikusanywa katika mwaka wa fedha 2016/17. Kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 7.5.
Katika mwezi Juni, 2018 pekee TRA imekusanywa jumla ya shilingi trilioni 1.5 ikilingishwa na shilingi trilioni 1.4 kwa mwezi juni, 2017 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.0.
Aidha TRA imetoa pongezi na shukrani kwa walipakodi wote ambao mchango wao umeiwezesha Serikali kupata mapato hayo ambayo yatasaidia katika shughuli mbalilmbali za maendeleo ya jamii yakiwemo ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara, ununuzi wa ndege, upatikanaji wa elimu, afya na mambo mengine kwa manufaa ya watanzania wote.
Tazama Video hapa chini kumsikiliza mKurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard M. Kayombo.