Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa chama chake kinapitia wakati mgumu sana kuwavumilia Chadema.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kitendo cha mgombea wa kiti cha Ubunge wa jimbo la Ukonga kumkaba koo msimamizi wa uchaguzi si cha kiungwana.

Amesema kuwa chama cha mapinduzi CCM kinapata wakati mgumu sana kavumilia vitendo kama hivyo ambavyo vinaenda kinyume na sheria.

“Kwakweli mgombea wa Chadema jimbo la Ukonga alichokifanya ni kitendo cha aibu, haiwezekani kumkwida msimamizi wa uchaguzi hadharani, hiyo ni aibu kubwa sana,”amesema Polepole

Tuzo Fifa: Luka Modric apewa nafasi, wapinzani wake watupwa
Paul Pogba aponda mfumo wa Jose Mourinho