Mbunge wa Babati mjini, Pauline Gekul amefunguka utofauti katika utendaji kazi alivyokuwa mbunge kwa kiti cha Chadema na utendaji kazi akiwa ndani ya Chama tawala CCM.

Akizungumza na mwandishi wa Dar24, Mercy Mbaya amesema kwa sasa masuala ya wananchi yanaenda vizuri sana na kazi imekuwa nyepesi tangu ahamie CCM.

”Nilivyohamia CCM nimepata ushirikiano wa hali ya juu sana masuala ya wananchi yanakwenda vizuri sana mwanzoni nilivokuwa mbunge wa upinzani vitu vingi manake nisukume mwenyewe  vinaweza visitekelezwe au visifanyike, lakini sahivi nipo CCM mambo yamekuwa rahisi sana” amesema Mbunge Gekul.

Ameongezea ndani ya CCM kuna mgawanyo mzuri wa kazi na kila kiongozi anafanya majukumju yake tofauti na alivyokuwa upinzani ambako Mbunge hubeba majukumu ya viongozi wa ngazi mbalimbali.

”Huko nilikotoka Mbunge ndio kila kitu wewe ndiyo mwenyekiti, wewe ndiyo mwenyekiti wa mtaa, wewe ndiyo katibu, wewe ndiyo everything, lakini huku nimeona kwamba kuna system ya cham amajukumu ya kichama yanafanyika zaidi na viongozi wa chama” amesema Gekul.

Bofya hapa chini kumsikiliza zaidi.

Jeshi la Sudan kuongoza nchi miaka miwili
LIVE MOROGORO: Mdahalo wa Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine