Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Shirikisho la Madereva Tanzania (TDF), Abdalah Lubala amesema kuwa leo wamekutana na Vyama vya Madereva nchini kwa ajili ya kuunda Katiba na kuchagua viongozi mbalimbali watakao ongoza shirikisho hilo kwa muda wa miaka minne.

Amesema hayo leo Septemba 15, 2018 Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kuundwa kwa Katiba na kufanya chaguzi mbalimbali za viongozi  kutasaidia  kutatua kero mbalimbali zinazo wakumba Madereva nchini Tanzania.

“Hili tunatekeleza agizo la Rais Dkt, John Magufuli alipotuambia kuunda chombo kitakachosaidia kutatua kero,” amesema Lubala

 

Shirikisho la Madereva Tanzania (TDF) lapata uongozi mpya
Aliyesaka mtoto kwa miaka 15 aweka historia ya kuzaa mapacha 5

Comments

comments