Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya fedha kuwafuta kwenye orodha ya mishahara wafanyakazi wa Serikali 9,932 waliobainika kuwa na vyeti bandia vya elimu.

Rais Magufuli amesema hayo baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti kwa wafanyakazi wa umma leo Aprili 28, 2017 katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma ambapo kwa mujibu wa ripoti hiyo takriban wafanyikazi 9,932 wa Serikali wana vyeti ghushi vya shule.

Rais Magufuli amewaagiza wafanya kazi wote walioghushi vyeti kuwacha kazi ifikiapo Mey 15 la sivyo wakamatwe na kushtakiwa.

Aidha, Rais Magufuli amezindua sherehe ya kutimiza miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kilianzishwa mwaka 2007.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 29, 2017
Sergio Aguero Amchefua Jose Mourinho