Wafuasi wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wameandamana nje ya mahakama kuu mjini Nairobi, wakiitaka majaji waliotoa uhamuzi wa kubatilisha ushindi wa Uhuru Kenyatta wachunguzwe.

Majaji wa mahakama hiyo walitoa uamuzi wa kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 mwezi Agosti yaliyompatia ushindi Kenyatta baada ya kusema kuwa mchakato wake ulitawaliwa na ukiukaji wa sheria.

Wafuasi wa Jubilee wanadai kuwa majaji wawili wa Mahakama kuu, Philemona Mwilu na Isaac Lenaola, ambao waliobatilisha matokeo ya uchaguzi huo walikutana na mawakili wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga, wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta.

Tazama video ya habari iliyorukwa na lituo cha KTN cha Kenya hapa chini;

Kichanga chaokotwa na ujumbe mzito
Bombardier yapata hitilafu Jijini Mwanza