Wakali watatu wa michano, P The MC, Zaiid na Wakazi ambao wameamua kuunda kikosi kazi cha kupiga muziki mzuri walichokibatiza jina la ‘SSK’ yaani Sisi Sio Kundi, wamefunguka jinsi walivyoweka mitego yao na shabaha ya kuianza kazi pamoja.

Wakifunguka katika mahojiano maalum na Dar24, SSK wamesema kuwa wazo la kufanya kazi pamoja lilianzia kwenye kazi ya Sijamoka, wamesema kuwa waliamua kuunganisha nguvu za kuwakusanya pamoja mashabiki wao na kisha kuwapa muziki mzuri kwa lengo la kufika mbali zaidi.

Mihimili hiyo mitatu ya michano mikali na ushairi unaoikuna mitaa hususan vijana wanaopenda muziki mzuri wameeleza jinsi watakavyokuwa wanaangusha makombora yao, ikiwa ni pamoja na albam yao ambayo iko mikononi mwa mtayarishaji Sijamoka.

Wameeleza kwa undani kuhusu mpango wao ambao ndani ya kipindi cha miezi miwili watakuwa wameteka mawimbi ya radio na kutikisa mara kadhaa spika za wapenda muziki mzuri.

Angalia video hii uwapate vizuri SSK na kile walicholenga:

P-Funk aeleza rapa wa Marekani MIMS alivyompa jina la kundi lake ‘Bongolos’
Sakata la Mkataba wa Simba na SportPesa Lazidi kuibua Mapya