Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amekemea vikali adhabu ambazo zimekuwa zikitolewa na walimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa kama walimu hao watashindwa kuendana na utaratibu uliowekwa ni bora wakakaa pembeni kuliko kuendelea kutoa adhabu zisizokuwa na tija.

“Hawa Walimu ni bora wakakaa pembeni, nimemuagiza naibu waziri wangu kukutana na uongozi mkoa wa Kagera kushughulikia suala hili, kwakweli ni suala linamsikitisha kila mtu hasa mimi kwakweli limenisikitisha sana,”amesema Jafo

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 2, 2018
Video: Nape amchana Prof. Jay, asema hana jipya