Wananchi wamezungumzia mwenendo wa hali ya kisiasa nchini ambapo wamesema kuwa elimu kuhusu masuala ya siasa inahitajika.
Wamesema hayo walipokuwa wakizungumza na Dar24 Media katika kipindi cha Sauti Zetu, ambapo wengi wao wamedai kuwa uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi ndio unaochangia kuleta taswira mbaya katika mwenendo wa siasa hapa nchini.
“Ili kila mmoja aweze kupata haki yake ya msingi ni lazima wananchi wapatiwe elimu itakayowafanya kuelewa haki zao za msingi na kuitumia ipasavyo,”amesema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ladislaus.