Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuswekwa ndani na kupelekwa mahakamani kwa watu ambao wamekuwa wakisema vyuma vimekaza na wale ambao wamekuwa wakisambaza takwimu mbalimbali za kupikwa.

Ameyasema hayo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma na kuwataka wananchi kuwa makini na masuala ya takwimu pia amewataka kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza ili hali watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka.

“Ukikosea kutoa takwimu umeichafua nchi, takwimu ni kitu kibaya sana ndiyo maana kuna watu wamebobea kwenye takwimu hivyo wananchi tuwasikilize watu wa takwimu asitokee mtu mwingine akatoa takwimu tofauti na zile walizonazo watu wa takwimu. Mtu anasema vyuma vimekaza wakati watu wa takwimu wanasema vyuma vimefunguka watu hawa wanatakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani ili wakajifunze kutoa takwimu huko,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, mbali na hilo Rais Dkt. Magufuli amewataka wananchi na taasisi mbalimbali wakitaka takwimu yoyote ile waende ofisi ya Takwimu na wasithubutu kutoa takwimu ambazo zinapingana na zile zilizopo ofisi ya takwimu

Mgombea ubunge Chadema ajitoa uchaguzi mdogo
Panga la moto kuwashukia wahubiri kwenye mabasi