Tangu tukiwa wadogo tumekuwa tukifundishwa umuhimu wa kuwa na imani sambamba na kumuamini Muumba ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kanisani ili kupata muongozo wa imani zetu.
Na imekuwa kawaida kuwaamini viongozi wetu wa dini pasipo kuwadharau lakini kwa sasa muda umekwenda na kumekuwapo na makanisa pamoja na wachungaji au viongozi ambao wameanzisha utaratibu unaoweza kukuacha ukishangaa na kuona sio sawa kwenye jamii.
Kutokana na matatizo na changamoto ambazo binadamu anakutana nazo kila siku watu wengi wamekuwa wakitafuta njia mbadala na njia mbalimbali za kutatua changamoto hizo ikiwa pamoja na kufuata maagizo wanayopewa na viongozi wa makanisa wanayosali, hali ambayo imeibua imani nyingi na za kustaajabisha.
Leo nimekuandalia makanisa yenye imani za kustaajabisha zaidi duniani katika kipindi chako pendwa cha Zaidi.