”Hali kwa sasa imekuwa ngumu sana tofauti na zamani, hakuna wateja kabisa na maua yanakauka kutokana na kukosa maji…,” hayo ni maneno ya mzee Rashid Bakari Kumbuti mmoja kati ya mauza wa miaka mingi ambaye kwa sasa ameeleza ugumu wa biashara hiyo akitofautisha na zamani.

Wakati akiongea na Dar24.com katika bustani yake Mbuyuni jijini Dar es salaam, Mzee Kumbuti ameseam zamani alikuwa akiuza maua ya shilingi laki tatu, nne hadi laki tano kwa siku lakini hali ya sasa imekuwa tofauti kwani amebahatika kuuza sana ni shilingi elfu ishirini hadi elfu kumi na tano kwa siku hali inayomfanya aanze kufikiria biashara nyingine.

Mbali na hayo Mzee huyo amesema bustani nyingi zinakauka kutokana na kukosa maji kwani wanashindwa kulipa gharama za maji kutokana na biashara kusimama, hivyo ameiomba Serikali kuwaangalia kwani kutokana na kazi yao wamekuwa wakipanda miti na kutengeneza mazingira kuwa mazuri, hivyo Serikali inapaswa kuwaangalia kama watu muhimu kwa mazingira.

Kuhusu baadhi ya wauza maua kuhamia sehemu za bustani zao kama makazi, Mzee Kumbuti amesema siyo kweli ila saa nyingine wanapaswa kuwepo hadi usiku mkubwa kutokana na wezi wa maua yao hivyo wanabakia kulinda bustani zao kwani wanashindwa gharama za kulipa walinzi. Pia amezungumzia kuhusu baadhi ya maua kutajwa kuwa na sumu ambapo ameeleza kuwa yapo ila huwa kabla mteja hajanunua anafahamishwa kuhusu maua hayo na jinsi ya kujikinga nayo ila yasilete madhara.

Sallam aelezea collabo mpya ya Diamond, Rick Ross na Rihanna
Dimitri Payet Azigonganisha Arsenal, Man Utd