Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limemtaka Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kufuta kauli aliyoitoa kwenye Sala ya Eid el Fitr, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Jumatatu iliyopita Juni 26.

Mzee Mwinyi alisema kuwa anampongeza Rais Magufuli kwa jinsi anavyoinyoosha nchi, na kusema kama isingekuwa kubanwa na Katiba, alitakiwa aachwe atawale milele.

‘Kauli hii imetusikitisha sana hasa kuona inatolewa na mzee tena aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi yetu kwa miaka 10 na ambaye anatakiwa apime madhara ya kila neno analolitamka,”amesema Lutembeka

Wazee hao wamewataka wazee wenzao wa CCM, kujitokeza hadharani na kukaa na mzee Mwinyi na kumuonya kuhusu kauli zake hizo, huku wakiwataka pia wazee wa CCM kuungana nao, kukaa na Rais Magufuli na kumuonya Mzee Mwinyi.

 

Magazeti ya Tanzania leo Juni 30, 2017
Video: Dawa za Kulevya sasa kuwa historia nchini