Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amelijibu jeshi la polisi kuhusu kauli waliyoitoa kuwa jeshi halifanyi kazi kwa matamko ya wanasiasa.
Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Cloudstv.
Amesema kuwa askari aliyetoa kauli hiyo alipotoka na hajui utaratibu wa kiutendaji kazi serikalini hivyo kama angeamua kumueleza rais, basi askari angeweza kupoteza ajira yake.
“Yule askari sijui ni nani alimtuma kwenda kusema vile, nadhani alipotoka hajui utaratibu wa utendaji kazi serikalini, yeye hapaswi kujibu chochote, anatakiwa apokee maelekezo na kuyafanyia kazi,”amesema Waziri Dkt. Kigwangalla