Wizara ya maliasili na utalii leo septemba 5, 2016 imepokea msaada wa magari kumi kutoka katika shirika la Frankfurt Zoological Society kwaajili ya kuimarisha na kupambana na majangili ambao wana hatarisha maisha ya wanyama ambapo kila siku wamekua wakipungua.

Waziri wa maliasili na utalii, Jumanne Maghembe alilishukuru shirika hilo kwa kutoa msaada huo kwani na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia sekta hiyo kwani ni sekta ambayo ni muhimu sana katika kuhakikisha wanyama wanalindwa .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo hapa nchini, Gerald Bigurube amesema wameamua kutoa msaada huo ili kuweza kuchangia kuokoa maisha ya wanyama na kusaidia kutatua tatizo la uwindaji haramu unaofanywa na watu wasiokua na nia njema. Tazama hapa video

Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Wananchi Watakiwa Kutoa Maoni Kuhusu Uendeshaji wa Serikali Kwa Uwazi
Video: Waziri Makamba Apokea Kamati Ya Mazingira Kutoka Sweden