Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba ameipokea kamati  inayoshughulikia mazingira kutoka nchini  sweden, kamati hiyo ilimtembelea ofisini kwake leo Septemba 5, 2016 na kufanya naye mazungumzo.

Makamba amesema kuwa Sweden imekua mdhamini mkubwa wa Baraza la usimamizi wa mazingira nchini NEMC ambapo tangu mwaka 1984 sweden imekua ikisimamia na kushirikiana na Baraza hilo katika shughuli zote zinazohusu mazingira.

Kamati hiyo ya Mazingira  iliambatana na balozi wa Sweden hapa nchini Bi. Katarina Rangnitt ambapo kwa upande wake alisema wanafanya kazi kwa muda mrefu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ya mahusiano madhuri waliyonayo tangu enzi na enzi hivyo inawapelekea kuzidi kudumisha uhusiano huo kwa kufanya kazi kwa pamoja. Bofya hapa kutazama video

Video: Waziri Maghembe apokea msaada wa magari 10 kutoka Frankfurt Zoological Society
Video: Kamanda Sirro atoa taarifa ya ujambazi, Watatu wakamatwa na silaha 23, risasi 835