Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa  makazi mapya ya Waziri Mkuu katika eneo la Mlimwa na kuagiza umalizike kwa wakati ili aweze kuhamia kama alivyoahidi.

Katika ziara hiyo aliyoifanya leo mchana (Jumatano, Septemba 7, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na namna kazi ya ujenzi inavyofanyika.

Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa bali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.

Waziri Mkuu amesema tayari Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina mpango kamambe (master plan) na ina viwanja vya kutosha kujenga makazi na ofisi mbalimbali. Tazama hapa video

TACAIDS Imeyataka Mashirika na Taasisi Kuepuka Kujiingiza Kwenye Unaharakati Kinyume cha Sheria
Australia yatwaa ubingwa mpira wa magongo kimataifa