Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameeleza kushangazwa na shutuma dhidi yake na Serikali kuwa wamekamata kazi feki za wasanii na baadaye kuzirudisha kwa wamiriki wa kazi hizo kupitia milango ya nyuma.
Nape amesema hayo wakati alipotembelea ghala la Kampuni ya Udalali ya YONO, ambapo amewatoa wasiwasi wasanii na kuwaeleza kuwa bidhaa hizo za muziki na video zipo mahali salama na zitateketeza bila kificho muda si mrefu.
Aidha, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifamba amewaasa wasanii kuacha tabia za kuwashutumu viongozi bila kuwa na ushahidi wa kutosha.